Baada ya kutokewa na ajali ya moto
katika hostel za Mabibo, ofisi ya waziri mkuu DARUSO nayo ikawaka moto
wakati waziri mkuu akiwa mabibo kushughulikia janga la moto lililotokea
huko.
Chanzo cha habari yetu kimeeleza kuwa
Naibu Spika wa bunge la DARUSO amesema kuwa moto huo inawezekena ukawa
umesababishwa na shot ya umeme kwa sababu ofisi ilikuwa imefungwa na
kulikuwa hakuna mtu.
Ifahamike kuwa ofisi hiyo iko mbali kabisa na hostel za mabibo na eneo jingine tofauti kabisa.
Chanzo cha habari kimesema kuwa moto huo ulianza mida ya saa tatu usiku.
Chanzo cha habari kimesema kuwa moto huo ulianza mida ya saa tatu usiku.
"Nlikuwa MTU Wa kwanza kuanza kuuzima na
kwa kushirikiana na Mbunge Tumsifu Robert tukapta ushirikino toka kwa
wakaazi Wa hall 6 na 7 tukiwa nje tukafanikiwa kuuzima moto baada ya
kuvuja baadhi ya vioo katika office hiyo lakini ukweli ni kwamba
tuwaachie wataalam waseme chanzo lakini nikifa leo niache ujumbe huu "
Moto ule umesababishwa na sababu nyingine Nje na shoti ya umeme" alieleza shuhuda wa tukio hilo.
Kwa bahati nzuri moto ulidhibitiwa na
hivyo ni makochi ya kukalia wageni tu ndiyo yaliyoungua na kuziacha
document na kiti na meza ya Waziri Mkuu vikiwa salama.